Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 06:28

Umoja wa Ulaya kuwawekea vikwazo wahusika wakuu katika vita ya Sudan


Moto mkubwa katika Mnara wa Kampuni ya Mafuta ya Greater Nile huko Khartoum Septemba 17. Picha na AFP.
Moto mkubwa katika Mnara wa Kampuni ya Mafuta ya Greater Nile huko Khartoum Septemba 17. Picha na AFP.

Mabalozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana juu ya muundo wa vikwazo ambavyo vitatumika kuwalenga wahusika wakuu katika vita vya Sudan na kuzuia mali zao na marufuku ya kusafiri, vyanzo vinavyofahamu suala hilo vimesema.

Vita vilizuka nchini Sudan mwezi Aprili mwaka huu kati ya jeshi, wakiongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ambaye alimuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir mwaka 2019, na kikosi cha wanamgambo kinachoongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana kama Hemedti.

Mapigano na umwagaji damu umeendelea kuenea licha ya majaribio ya kimataifa ya kupata sitisho la kudumu la mapigano. Vita vimewabandua zaidi ya watu milioni tano kutoka katika makazi yao na kusababisha janga la kibinadamu, wakati madaktari wa eneo hilo wakionya kuhusu kusambaa kwa magonjwa ya kipindupindu na homa ya dengue.

Pendekezo la vikwazo liliwasilishwa mwezi Julai lakini halikuidhinishwa hadi Jumatatu. Mawaziri wa mambo ya nje wa EU bado wanahitaji kufanya maamuzi ya mwisho baadaye mwezi huu kabla ya umoja huo kuanza kuongeza watu binafsi na vyombo kwenye orodha hiyo.

Marekani, Uingereza, Norway na Ujerumani zinapanga kuwasilisha hoja katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ili kuanzisha uchunguzi kuhusu madai ya ukatili nchini Sudan, ikiwa ni pamoja na mauaji yaliyochochewa na ukabila, rasimu ya hoja ilionyesha Ijumaa.

Chanzo cha habari ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG