Moto uligubika mji mkuu wa Sudan siku ya Jumapili na vikosi vya kijeshi vilishambulia makao makuu ya jeshi kwa siku ya pili mfululizo, mashahidi waliripoti, wakati mapigano yakiingia mwezi wa sita.
Mapigano ya sasa yanatokea karibu na makao makuu ya jeshi huku kukiwa na aina mbalimbali za silaha, walioshuhudia waliiambia AFP Jumapili kutoka Khartoum, huku wengine wakiripoti mapigano katika mji wa El-Obeid, kilomita 350 Kusini.
Mapigano kati ya jeshi la kawaida na Vikosi vya Msaada wa Haraka vya kijeshi yaliongezeka Jumamosi, na kusababisha majengo kadhaa muhimu katikati mwa Khartoum kushika moto.
Forum