Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 00:21

UNHCR yahofia mzozo wa Sudan kuzidi kuleta maafa


Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Jumatano limeonya kwamba dharura ya kibinadamu ya Sudan iliyochochewa na mvutano wa majenerali wawili wenye upinzani na kupigania udhibiti wa nchi hiyo imezua mzozo mkubwa wa kibinadamu.

Mzozo huo upo ndani ya Sudan na katika nchi jirani zinazo wapa hifadhi wakimbizi, mzozo ambao una hatari wa kuyumbisha utulivu wa kanda hiyo kadiri mzozo unavyoendelea.

“Popote pale duniani ambapo mzozo unazidi kuendelea, na Sudan kuna uwezekano kuzidi kuendelea, itafanya kuwa moja ya orodha yangu ndefu ya matatizo ya muda mrefu,” alisema Ayman Gharaibeh, mkurugenzi wa ofisi ya UNHCR ya kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.

Karibu ya watu milioni 6 nchini Sudan wamefurushwa kutoka makaazi yao toka mapigano kuanza katikati ya Aprili, na kufanya kuwa mzozo wa sasa kabisa uliosababisha wakimbizi kwa haraka zaidi duniani.

Forum

XS
SM
MD
LG