Ukosefu wa mafuta wasababisha taharuki Uingereza

Kituo cha mafuta kimefungwa mjini London, Sept. 30, 2021.

Vituo vingi vya mafuta nchini Uingereza bado vimefungwa Ijumaa kutokana na ukosefu wa mafuta kufuatia wiki nzima ya taharuki iliyoshuhudiwa watu wakijaribu kununua mafuta na hata kupigana kwenye vituo hivyo. 

Madereva walionekana wakijaza mafuta wakiyatia ndani ya chupa za maji baada ya kutokea upungufu wa madereva wa malori kusafirisha mafuta hadi vituoni.

Upungufu wa mafuta kufuatia Brexit, Uingereza kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya na janga la COVID-19 umezusha matatizo makubwa katika baadhi ya sekta za taifa kubwa la tano la kiuchumi duniani.

Mawaziri wa Uingereza kwa siku kadhaa wamekuwa wakisisitiza kwamba tatizo limepungua na hata kumalizika ingawa wauzaji rejareja wanasema zaidi ya vituo 2,000 havina mafuta.

Shirika la habari la Reuters lina ripoti kuendelea kufungwa kwa vituo vingi mjini London na kusini mwa Uingereza.

Chanzo cha habari hizi ni shirika la habari la AP