Jaji Baraister anasema amechukua uamuzi huo kutokana na hatari ya uwezekano wa Assange kujiua.
Jaji huyo ameeleza kwamba endapo Assange atapelekwa Marekani ambaye ni Muaustralia atakabilwa na hali ya kushikiliwa katika mazingira magumu ya kumtenganisha na watu na mawasiliano na watu wa nje na hivyo kumuathiri kiakili na kwa hiyo aliamrisha asipelekwe Marekani.
Assange mwenye umri wa miaka 49 anaendelea kushikiliwa hadi pale ombi lake la kuachiliwa kwa dhamana litaposikilizwa Jumatano.
Waendesha mashtaka wa Marekani na Uingereza wanaweza kukata rufaa kutokana na uamuzi huo. Mawakili wake wametoa hoja kwamba kesi dhidi yake ina malengo ya kisiasa.