Mamlaka ya ulinzi wa fedha Uganda – iliowekwa kuzuia mizunguko ya fedha haramu – inasema inaukosefu wa rasilmali kuweza kuzuia miamala hiyo batili.
Ukwepaji wa kodi, utakatishaji wa fedha na mambo mengine yanayo fungamana na ufisadi, vinaigharimu Uganda kiasi cha fedha kisichopungua bilioni moja ya dola za Marekani kila mwaka, kwa mujibu wa taasisi ya fedha ya kimataifa ya maadili (Global Financial Integrity).
Taasisi isiyo tengeneza faida yenye makao yake Washington DC imesema katika Ripoti yake ya Septemba kuwa ukwepaji kodi unaotokana na kusafirisha na kuingiza bidhaa nchini peke yake zimeigharimu Uganda dola za Marekani bilioni 6.7 katika kipindi cha mwaka 2006-2015.
Takriban dola za Marekani bilioni 3 zaidi zimepotea kutokana na makosa ya kihesabu na kusahauliwa kuwekwa katika rikodi za malipo kwa kipindi cha muongo uliopita.
GFI inasema hasara ya kiuchumi iliongezeka kutokana na Uganda kuwa ni kichaka cha mzunguko wa fedha haramu kutoka nchi jirani zilizo sambaratishwa na vita, kama vile Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Somalia na Kenya.