Uchumi wa Niger wazorota

Wafuasi wa Baraza la Kitaifa la Ulinzi la Nchi ya Niger (CNSP) wakifanya maandamano nje ya kambi ya jeshi Niger na Ufaransa Septemba 2, 2023. Picha na AFP

Uchumi wa Niger bado unaendelea kukua taratibu licha ya kuondolewa vikwazo vigumu wiki mbili zilizopita katika taifa hilo linaongozwa kijeshi, na magenerali hawajaonyesha nia yoyote ya kufungua mipaka yake na Benin na kutafuta suluhu ya kidiplomasia na mataifa jirani

Vizuizi awali viliwekwa kwa matarajio ya uingiliaji kati kijeshi wa ECOWAS na bado barabara inayounganisha Niger na Benin imefungwa.

Mzozo wa kisiasa na kiuchumi baina ya Niamey na ECOWAS ambayo inataka kuachiliwa kwa rais aliyoondolewa madarakani Mohamed Bazoum na kurejeshwa utawala wa kikatiba umesalia tangu mapinduzi ya julai yaliyomng’oa madarakani.

Jumuiya ya ECOWAS ilitangaza mwezi Februari mwishoni ilikuwa inaoondoa vikwazo vilivyoharibu zaidi, ikiwa ni pamoja na eneo lenye marufuku ya kurusha ndege, kufungwa mipaka na kufungia mali.