Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:03

Wanajeshi wa Niger wauawa karibu na mpaka wa Nigeria


Watoto waliopoteza makazi wakiwa katika kijiji kilichopo Kusini Kaskazini mwa Niger Juni 9, 2022. Picha na BOUREIMA HAMA / AFP.
Watoto waliopoteza makazi wakiwa katika kijiji kilichopo Kusini Kaskazini mwa Niger Juni 9, 2022. Picha na BOUREIMA HAMA / AFP.

Wanajeshi wanne wa Niger wamefariki wakati wa uvamizi wa alfajiri uliofanywa na darzen ya washambuliaji wenye silaha katika eneo lililo jirani na mpaka wa Nigeria, television ya taifa ilitangaza Ijumaa.

“Idadi kubwa ya watu wenye silaha walikuja wakiwa katika pikipiki zipatazo 100 na kuwashambulia polisi” katika kituo cha Bassira, kwenye kijiji cha mpakani, katika mkoa wa Maradi, afisa aliyechaguliwa wa eneo hilo ameliambia shirika la habari la AFP.

Shambulio hilo limesabaisha vifo vya watu wanne na wawili wamejeruhiwa miongoni mwao ni wanajeshi jeshi la Ulinzi na Usalama la Niger (FDS) Shirika la Utangazaji la serikali limeripoti, wakati mwanamke mmoja amejeruhiwa na risasi iliyompitia kwa bahati mbaya.

Baada ya kufyatuliana risasi kwa muda wa saa moja, FDS waliwazidi nguvu washambuliaji ambao walichukua maiti na majeruhi, lakini walitelekeza pikipiki tatu, vifaa vya mawasiliano na risasi, kulingana na ripoti hiyo.

“Ni shambulio ambalo halikutarajiwa katika eneo hilo” afisa aliyechaguliwa alisema , ambapo watu hao wenye silaha wanaoitwa “majambazi” mara nyingi huua, hupora na kutisha watu.

Eneo hilo linahifadhi wakimbizi wa Wakinigeria zaidi ya 46,000, waliokimbia ghasia za magenge yenye silaha ambayo yamekuwa yakiutishia mpaka kwa miaka mingi, kulingana na takwimu rasmi.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG