Ripoti kwenye tovuti ya gazeti la Uingereza Telegraph, inaeleza zaidi juu ya baadhi ya mambo yaliyo gunduliwa kwamba “masoko yenye misongamano, madarasa ya kujifunza kudansi, mabaa yenye makelele na kuimba kwa sauti kubwa” inawezekana ikawa ni mambo yanayo changia kueneza virusi vya corona.
Umma tayari unafahamu kuwa maeneo yenye kupelekea “maambukizi makubwa” ni pamoja na “hospitali, nyumba za kuleya wazee, mabweni makubwa, viwanda vya kutengeneza vyakula na masoko ya vyakula.”
Lakini moja ya eneo lenye kueneza maambukizi, kwa mujibu wa Makala hiyo, inatokana na baa huko Tyrolean Alps. Gazeti la Telegraph limesema mamia ya maambukizi huko Uingereza, Ujerumani, Iceland, Norway na Denmark yamethibitishwa kutokea katika baa ya Kitzloch, inayofahamika kwa sherehe zake baada ya michezo katika thaluji.
Utafiti huko Korea Kusini uligundua pia kuwa “mazoezi ya nguvu ya viungo katika nyumba za mazoezi zilizo na msongamano zinaweza kuongeza hatari ya maambukizi” ya virusi vya corona.
Utafiti huo uligundua kuwa watu 112 waliambukizwa na virusi hivyo katika siku 24 baada ya kushiriki katika “mafunzo ya dansi yenye mahadhi ya muziki wa Kilatini” katika maeneo 12 mbalimbali yanayotoa mafunzo.
Katika utafiti mwengine, wanakwaya walikutikana kua na uwezekano wa kuambukizwa virusi hivyo, lakini wanasayansi wanaamini kuimba siyo njia pekee ya kueneza maambukizi katika kipindi cha siku za awali za maambukizi kabla ya utaratibu wa kutosogeleana kufuatwa.
Virusi hivyo vya corona huwenda vilienezwa wakati wanakwaya walipokuwa wakisalimiana, wakibadilishana vinywaji na “huku wakiongea kwa kukaribiana.”
Maelezo ya gazeti hilo yamesema virusi hivyo viliwavamia waimba kwaya Amsterdam, na kuwaambukiza wanachama wake 102 kati ya 130.