Siku ya Wakimbizi Duniani yasherekea ujasiri na uvumilivu wa wakimbizi

Mkimbizi kutoka Somalia Faiza Abdulahi Hassan na watoto wake watanno atapewa makazi mapya Marekani baada ya kuishi kwa muda wa miaka mitano katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab. Picha na Bobb Muriithi/AFP.

Siku ya Wakimbizi duniani, ambayo huadhimishwa Juni 20, mwaka huu siku hii inasherehekea ujasiri, uvumilivu, na ushujaa wa mamilioni ya watu ambao wanazikimbia nchi zao ili kuepuka migogoro au mateso.

Kijana mmoja aliyekuwa mkimbizi na ni mjasiriamali amejaribu kuzigeuza hadithi za wakimbizi kuwa kitu cha kuwatia moyo watu wengine waliokimbia makazi yao.

Mohamed Malim mwenye umri wa miaka 27, ambaye alikuwa mkimbizi kutoka Somalia na baadaye kuwa mjasiriamali wa kijamii, ni mkurugenzi wa chapa ya mitindo ya mavazi ya Epimonia, kampuni ndogo iliyoko Minnesota ambayo aliianzisha mwaka 2018.

Kampuni hiyo inakusanya majaketi ya kuokoa maisha ambayo wakimbizi wamekuwa wakivaa, na mabaki ya mitumbwi dhaifu waliyoitengeneza wenyewe kutoka katika fukwe za Ugiriki, na kuvigeuza vipande hivyo vya safari ya wakimbizi kuwa kitu kinachoonekana zaidi.

"Tunachukua majaketi ya kuokoa maisha ambayo wakimbizi wameyavaa wakivuka Bahari ya Mediterranean na kuyageuza kuwa vipande vya mitindo ili kuleta ufahamu wa mzozo wa kimataifa wa wakimbizi, na kusaidia ubunifu wa wakimbizi, katika sanaa na mitindo," Malim aliiambia Idhaa ya Kisomali ya VOA.

Bidhaa hizo za kipekee za Epimonia ni bangili zinazong’ara zenye rangi ya chungwa zilizotengenezwa kutokana na mabaki ya majaketi ya kuokoa maisha yaliyotupwa ambayo wakimbizi waliyatumia kwenye safari yao.

Wahamiaji wakiwa wamepanda boti wakijaribu kuingia Ugiriki. Picha na Ozan KOSE / AFP.

Malim anasema vikuku vimeanza kuvaliwa kwenye mikono ya vijana nchini Marekani, hususani huko Minnesota, na kupata faida ambayo inarudi kwa wakimbizi.

"Tunasaidia wakimbizi kwa kuwapatia ajira, kusambaza mwamko, na kuchangia asilimia 50 ya faida tunayoipata kwenye mashirika ya Marekani ambayo yanawasaidia wakimbizi kwa kuwapa fursa ya kupata za elimu na maendeleo," alisema Malim.

Malim alikuwa mkimbizi, alizaliwa katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya. Alikuwa na umri wa miaka minne wakati familia yake ilipohamia Marekani mwaka 1999.

"Kwanza tulifikia Texas na kisha tukahamia Minnesota, ambako safari nilizopitia zilinitia moyo ya kutaka kuleta mabadiliko duniani, haswa kwa wakimbizi wengine," alisema. "Kwa kweli ninashukuru sana kwa hapa nilipofikia, mahali ambapo ninaweza kuwasaidia wakimbizi wenzangu kutimiza ndoto zao na matumaini yao."

"We support refugees through providing employment, spreading awareness, and donating 50% of our profit to U.S. organizations that support refugees with opportunities for education and advancement," said Malim.

"Tunasaidia wakimbizi kwa kuwapatia ajira, kusambaza mwamko, na kuchangia asilimia 50 ya faida tunayoipata kwenye mashirika yaliyoko Marekani ambayo yanawasaidia wakimbizi kwa kuwapa fursa ya kupata za elimu na maendeleo," alisema Malim.

Malim alikuwa mkimbizi, alizaliwa katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya. Alikuwa na umri wa miaka minne wakati familia yake ilipohamia Marekani mwaka 1999.

"Kwanza tulifikia Texas na kisha tukahamia Minnesota, ambako safari nilizopitia zilinitia moyo ya kutaka kuleta mabadiliko duniani, haswa kwa wakimbizi wengine," alisema. "Kwa kweli ninashukuru sana kwa hapa nilipofikia, mahali ambapo ninaweza kuwasaidia wakimbizi wenzangu kutimiza ndoto zao na matumaini yao."