Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:32

Wanamgambo washambulia kambi ya wakimbizi na kuua watu 41 mashariki mwa DRC


Kambi ya wakimbizi wa ndani ya nchi Ituri, Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Kambi ya wakimbizi wa ndani ya nchi Ituri, Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Wanamgambo walishambulia kambi ya wakimbizi kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuua watu 41, afisa wa wilaya ya Djugu amesema Jumatatu.

Wanamgambo wa kundi la CODECO walishambulia kambi katika mkoa wa Ituri mapema Jumatatu, Richard Dheda, afisa katika wilaya ya Djugu ameiambia AFP.

CODECO inadai kulinda jamii ya Walendu dhidi ya kabila la Wahema, pia dhidi ya jeshi la DRC.

“Walianza kwa kufyatua risasi, watu wengi waliuawa kwa kuchomwa moto ndani ya nyumba zao, wengine waliuawa kwa panga,” mwakilishi wa mashirika ya kiraia Desire Malodra amesema.

Kambi ya Lala inayohifadhi wakimbizi wa ndani inapatikana umbali wa kilomita 5 kutoka kijiji cha Bule ambako kuna kambi ya wanajeshi wa Umoja wa mataifa.

Mkoa wa Ituri ni mmoja ya maeneo ya mashariki mwa DRC yanayokumbwa na machafuko, ambapo mashambulizi yanayosababisha vifo vya raia ni ya kawaida.

Forum

XS
SM
MD
LG