Hali hiyo imesababisha serikali ya mpito kuanzisha utaratibu wa kutoa mafuta ili kujaribu kukabiliana na tatizo kubwa la kiuchumi linalotokana na ukosefu wa mafuta ya petroli.
Baadhi ya watu wamekuwa wakisimama kwa siku kadhaa kwenye mistari mirefu ya msongamano wa magari unaofikia takriban kilomita kadhaa tangu kuanza tatizo la upungufu wa mafuta mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kabla ya upungufu wa mafuta kulikuwepo na upungufu wa mkate jambo ambalo limesababisha hali ngumu kwa serikali mpya inayojaribu kuleta mabadiliko na maisha bora baada ya kupinduliwa kwa Omar Al Bashir mwaka 2019.
Maafisa wa serikali wanasema upungufu wa mafuta hivi sasa unatokana na kuharibika kwa bomba la mafuta kutoka kiwanda cha kusafisha mafuta.
Zaidi ya hayo kusambaza mafuta na uagizaji wa bidhaa unakabiliwa na tatizo la upungufu wa fedha za kigeni na usafirishaji.