Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:24

Serikali ya Sudan na waasi wamesaini mkataba wa ratiba ya upatikanaji amani


Baadhi ya waandamanaji waliokuwa wakiipinga serikali ya Sudan mjini Khartoum, Januari 17
Baadhi ya waandamanaji waliokuwa wakiipinga serikali ya Sudan mjini Khartoum, Januari 17

Serikali ya Sudan na makundi tisa ya waasi Jumamosi wametia saini mkataba wa ratiba kuelekea kumaliza mgogoro wa umwagaji damu katika jimbo la Darfur. Mkataba huo umeelezea masuala mbali mbali ambayo vyama vitahitajika kushauriana wakati wa duru ya mazungumzo mjini Juba.

Mpatanishi mkuu wa matatizo ya Darfur, Ahmed Mohamed kutoka Sudan Revolutionary Front-SRF ushirika wa makundi tisa ya waasi yaliyoshiriki kwenye mazungumzo na serikali ya Sudan alisema tunaamini hii ni hatua moja muhimu. Mohamed aliliambia shirika la habari la AFP kwamba hakuna shaka hatua hii itasaidia utaratibu wa kufanikisha amani ya kudumu huko Darfur na pia utafanikisha utaratibu wa serikali ya mpito huko Sudan kusonga mbele kwa utulivu bila kuwepo vizuizi.

Baadhi ya makundi yaliyoandamana kuipinga serikali ya Sudan
Baadhi ya makundi yaliyoandamana kuipinga serikali ya Sudan

Miongoni mwa masuala waliyokubaliana ambayo yanahitaji kushughulikiwa ni kiini kinachosababisha mgogoro, kurudi kwa wakimbizi na watu waliokoseshwa makazi ndani ya nchi yao, kushirikiana madaraka na kushirikishwa kwa vikosi vya waasi ndani ya jeshi la taifa.

Mkataba huo pia unasema kwamba serikali ya Sudan itaelezea masuala ya ardhi kama vile kuharibiwa kwa mali wakati wa mgogoro. Khartoum imekuwa ikizungumza na makundi tofauti tofauti ya waasi katika mji mkuu wa Sudan Kusini kwa wiki mbili, katika duru ya mazungumzo ya karibuni katika juhudi za kumaliza migogoro huko majimbo ya Darfur, Blue Nile na South Kordofan.

XS
SM
MD
LG