Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 12:49

Sudan itampeleka Bashir mbele ya ICC


Rais wa zamani wa Sudan Omar Hassan al-Bashir akiwa ndani ya kizimba cha ulinzi ndani ya mahakama akikabiliwa na mashtaka ya rushwa njini Khartoum, Sudan August 19, 2019.
Rais wa zamani wa Sudan Omar Hassan al-Bashir akiwa ndani ya kizimba cha ulinzi ndani ya mahakama akikabiliwa na mashtaka ya rushwa njini Khartoum, Sudan August 19, 2019.

Utawala wa mpito wa Sudan umetangaza Jumanne kwamba utamkabidhi rais wa zamani Omar Al Bashir kwa mahakama ya uhalifu wa kimatiafa ICC.

Habari za kupelekwa The Hague zimetolewa baada ya mazungumzo katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba kati ya wajumbe wa serikali ya mpito ya Sudan na makundi ya waasi kutoka jimbo la Darfur.

Akizungumza na Sauti ya Amerika, Ahmed Tugod mwakilishi wa kundi la waasi la Vuguvugu la Haki na Usawa, JEM amesema pande zote zimekubaliana kuwakabidhi raia wanne wa Sudan walofunguuliwa mashtaka na ICC akiwemo Bashir.

Tugod anasema, makubaliano ya kuwakabidhi watu hao haitatekelezwa hadi pale makubaliano kamili ya amani yanafikiwa kati ya pande zote zinazo zozana huko Sudan kufikiwa.

Anasema wanataraji makubaliano hayo yatafikiwa mnamo wiki chache zijazo.

Rais huyo wa zamani anakabiliwa na mashtaka ya mauwaji ya halaiki, uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu kutokana na vita vilivyotokea katika jimbo la Darfur nchini mwake mnamo mwaka 2003.

Waendesha mashtaka wa ICC mjini The Hague, walitoa hati ya kukamatwa kwa al-Bashir baada ya kutofika mbele ya mahakama hiyo kukabiliwa na mashtaka ya mauwaji ya Darfur.

Umoja wa Mataifa unasema karibu watu laki tatu waliuliwa na watu milioni 2 na nusu walikoseshwa makazi yao kutokana na vita hivyo.

XS
SM
MD
LG