Walioshuhudia wamesema shambulio hilo liligonga ardhi ambayo haikaliwi na mtu, iliyoko kati ya milango ya Misri na Palestina, na kuharibu ukumbi wa upande wa Palestina.
Shirika la habari la AFP lilipowasiliana na, jeshi la Israel lilisema "haliwezi kuthibitisha au kukanusha" shambulio lolote lililotokea kwenye kivuko "wakati huu".
Kundi la Misri la Sinai kwa Haki za Binadamu limesema shambulio hilo lilisababisha kufungwa kwa kivuko hicho lakini hakuna uthibitisho uliopatikana kwa haraka kutoka pande zote mbili.
Ilikuwa ni mara ya pili kwa kivuko hicho kupigwa, tangu Israel ilipoanzisha mashambulia makali ya mabomu eneo la Gaza kujibu shambulizi la ghafla lililofanywa na watawala wa Hamas siku ya Jumamosi na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 900 nchini Israel.
Shambulio la awali la Jumatatu, lilisitisha kwa muda njia inayotumika katika kivuko hicho, chanzo cha usalama na mashahidi walisema.
Hakuna maoni yoyote kutoka mamlaka ya Misri.
Israel imetangaza "kuizingira kabisa" Gaza, kukata chakula, maji na usambazaji wa umeme kwa watu milioni 2.3 wa eneo hilo.
Chanzo cha habari ni Shirika la habari la AFP