Pia serikali hiyo iliyoko madarakani imeondoa sheria kandamizi zilikuwa zikitumiwa na Rais wa zamani Omar al Bashir dhidi ya wanawake.
Wakati wa utawaka wake, wanawake walikabiliwa na sheria kali za mavazi, uhuru wa kutembea, uhuru wa kufanya kazi pamoja na haki ya kupata masomo miongoni mwa mambo mengine.
Hatua hizo mbili zimechochewa na baadhi ya mambo yalioitishwa na vuguvugu la maandamano lililomuondoa Bashir madarakani mwezi Aprili 2019.
Kutekelezwa kwa sheria hiyo mpya kunaonyesha ari ya serikali ya mpito ya kuondoa baadhi ya sheria kandamizi zilizotumika wakati wa uongozi wa Bashir uliodumu kwa miongo mitatu.
Tangu kuchukua madaraka kwa njia ya mapinduzi 1989, Bashir alisimika sheria za Kiislamu kwenye taasisi nyingi nchini humo.
Kumalizwa kwa chama cha Bashir cha National Congress, NCP kuna maana kwamba mali zake sasa zitachukuliwa na serikali kulingana na Abdelbari.
Televisheni ya kitaifa imetaja hatua hiyo kuwa yenye lengo la kumaliza kabisa utawala wa zamani.
Waziri Mkuu Abdalla Hamdock kwenye ukurasa wake wa tweeter ameandika kwamba hatua hiyo siyo ya kulipiza kisasai mbali ni ya kurejesha hadhi kwa watu wa Sudan. wa.