Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 09:56

TMC na viongozi wa waandamanaji Sudan wamefikia mkataba wa serikali ya muda


Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo na kiongozi wa waandamanaji Ahmad al-Rabiah wakipeana mikono kwenye utiaji saini wa awali wa kushirikiana madaraka
Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo na kiongozi wa waandamanaji Ahmad al-Rabiah wakipeana mikono kwenye utiaji saini wa awali wa kushirikiana madaraka

Shirika la habari la Associated Press linaripoti mkataba utatiwa saini Jumapili. Pande hizo mbili zimefikia mkataba wa serikali ya muda itakayoongoza kwa kipindi cha miaka mitatu

Mpatanishi wa Umoja wa Afrika, Mohamed Hassan Lebatt alisema baraza la jeshi la muda nchini Sudan-TMC pamoja na viongozi wa waandamanaji wamefikia mkataba wa serikali ya muda kwa miaka mitatu ambayo itaongoza kupatikana utawala wa kiraia.

Lebatt alisema Jumamosi bila kutoa taarifa zaidi za kina, akieleza ninawatangazia wasudan, wa-Afrika na jumuiya ya kimataifa kwamba pande mbili zilizopo kwenye mazungumzo ya Amani nchini Sudan wamekubaliana kwa dhati juu ya mkataba wa kikatiba. Mazungumzo yanatarajiwa kuendelea kufanyia kazi zaidi masuala ya ndani.

Shirika la habari la Associated Press-AP linaripoti mkataba utatiwa saini Jumapili. Sudan imekuwa kwenye wimbi la maandamano kwa miezi kadhaa. Maandamano yalizuka kwanza mwezi Disemba kufuatia ongezeko la bei ya mafuta ya gari. Hatimaye yaliingia kuwa maandamano ya mabadiliko ya kisiasa yaliyopelekea kuondolewa madarakani Omar al-Bashir kwa njia ya mapinduzi April 11 mwaka huu.

XS
SM
MD
LG