Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 07:33

Marekani itaanza kuifuatilia Sudan iwapo inatimiza ahadi zake kwa raia


Viongozi wa serikali mpya ya mpito nchini Sudan wakati wakila kiapo mjini Khartoum. August 21, 2019
Viongozi wa serikali mpya ya mpito nchini Sudan wakati wakila kiapo mjini Khartoum. August 21, 2019

Ofisa mmoja mwandamizi wa wizara ya mambo ya nje Marekani alisema kama pande zote zinafanya kazi kikamilifu wataendelea na utaratibu wa haraka kuiondoa nchi hiyo katika orodha ya ugaidi

Marekani ilisema Jumatatu itafuatilia kwa karibu dhamira ya dhati ya serikali ya mpito ya Sudan katika kulinda haki za kibinadamu, demokrasia na amani kabla ya Washington kuamua iwapo iiondoe Khartoum kutoka orodha ya Marekani ya nchi ambazo zinafadhili ugaidi.

Ofisa mmoja mwandamizi wa wizara ya mambo ya nje Marekani alisema kama pande zote zinafanya kazi kikamilifu wataendelea na utaratibu wa haraka kuiondoa nchi hiyo katika orodha ya ugaidi.

Waziri Mkuu wa Sudan, Abdalla Hamdok
Waziri Mkuu wa Sudan, Abdalla Hamdok

Waziri Mkuu mpya wa Sudan, Abdalla Hamdok, mchumi anayefahamika aliapishwa kuongoza serikali ya mseto nchini humo ambapo uteuzi wake umefanyika miezi minne baada ya kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa zamani wa Sudan, Omar al-Bashir ambaye aliongoza nchi hiyo kwa takribani miongo mitatu.

Ofisa mwingine mwandamizi wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani aliongeza kusema kwamba Waziri Mkuu Hamdok alisema vitu sahihi kabisa na hivyo wanatarajia kushirikiana na serikali yake. Marekani itaanza kuangalia kwa makini ahadi za serikali hii ya mseto.

XS
SM
MD
LG