Satellite za Marekani zaonyesha athari ya mafuriko kituo cha nyuklia Korea Kaskazini

Mvua zilizonyesha Jumatano August 5, 2020, Pyongyang, Korea Kaskazini zimeathiri sehemu kubwa ya nchi hiyo na hivyo kuwepo wasiwasi kuwa zitaathiri maisha ya watu ambao tayari wanaishi katika umaskini. (AP Photo/Cha…

Shirika la utafiti la Marekani limesema kwamba picha za satellite zinaonyesha mafuriko ya hivi karibuni nchini Korea kaskazini, huenda yaliharibu nyumba zilizounganishwa na kinu kikuu cha kutengeneza silaha za nuclear nchini humo.

Watafiti wa wavuti wa 38 North, unaofuatilia masuala ya Korea kaskazini, wamesema picha za satellite zilizopigwa kati ya Agosti 6 na 11, zinaonyesha kituo cha utafiti wa sayansi cha Yongbyon ambacho kina mifumo ya kupooza silaha za nuclear kimeathiriwa na mafuriko hayo.

Eneo la Korea limeshuhudia mvua kubwa sana katika siku za hivi karibuni, mafuriko na maporomoko ya ardhi yakisababisha uharibifu mkubwa na vifo vya watu Korea kaskazini na kusini, Shirika la Habari la Uingereza Reuters limeripoti.

Kituo cha Yongbyong, kilicho karibu na mto Kuryong, kilomita 100 kaskazini mwa mji mkuu wa Pyongyang, Korea kaskazini, hutengeneza vifaa vya nuclear, kuchuja mafuta na madini ya Uranium, vinavyoaminika kutengenza silaha za nuclear.