Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema hakutishiwa kwa namna yoyote katika mazungumzo yake ya simu ya mwezi Julai na rais wa Marekani Donald Trump.
Baada ya mazungumzo hayo suala hilo liko katikati ya uchunguzi wa Wademokrat katika baraza la wawakilishi la kutaka kumfungulia mashtaka ya kumwondoa Rais Trump madarakani .
Zelenskiy aliwaambia waandishi wa habari kwamba alikuwa hana habari kwa wakati huo kama Rais Trump alikuwa amezuia mamilioni ya dola za Marekani za msaada wa kijeshi kwa nchi yake.
Trump kwa upande wake amesema aliamua kufanya hivyo ili kuwashinikiza Ukraine kupambana na rushwa.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.