Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:55

Kamati za Baraza la Wawakilishi kufanya kikao cha faragha na Balozi Volker


Balozi Kurt Volker
Balozi Kurt Volker

Watumishi kutoka katika kamati tatu za baraza la wawakilishi wanaofuatilia suala la kutaka kumfungulia mashitaka Rais Donald Trump kutokana na mazungumzo yake na rais wa Ukraine wanatarajia kufanya kikao cha faragha Alhamisi na balozi wa Marekani nchini Ukraine aliyejiuzulu hivi karibuni Kurt Volker.   

Maswali yao yanatarajiwa zaidi kulenga juu ya mazumgumzo ya simu ya mwezi Julai kati ya Trump na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy.

Pia wataangaza hatua alizochukuwa Volker baada ya simu hiyo na shughuli za wakili binafsi wa Trump Rudy Giuliani kuhusiana na madai kwamba Trump alimwekea shinikizo Zelenskiy kumchunguza makamu rais wa zamani Joe Biden.

Shutuma hizo zilikuja baada ya mtoa taarifa wa siri kutoa malalamiko wiki iliyopita ambayo alisema kwa mujibu wa maafisa wa White House kwamba Trump pia alimwekea shinikizo Zelenskiy kukutana au kuzungumza na watu ambao aliwataja kama wawakilishi wake binafsi juu ya masuala haya ambao ni Rudy Giuliani na mwanasheria mkuu wa Marekani William Barr.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG