Tinubu, aliyeingia madarakani mwaka mmoja uliopita aliondoa ruzuku ya miongo kadhaa ya mafuta ambayo ilisababisha bei kuwa chini na kushusha thamani ya sarafu, hatua iliyopelekea ongezeko la mfumuko wa bei kwa asilimia 33 .69 mwezi April, kiwango chake cha juu zaidi katika takriban miongo mitatu na kudidimiza mapato.
Katika hotuba kwa taifa kuadhimisha siku ya demokrasia, Tinubu alikubali kwamba hali ngumu imesababishwa na mageuzi, ambayo pia ni pamoja na viwango vya juu vya riba na kuondolewa kwa sehemu ya ruzuku ya umeme lakini alisema hii itaunda msingi mzuri wa ukuaji wa siku zijazo.
“ninaelewa hali ngumu ya uchumi tunaokabiliana nao kama taifa wakati huu, uchumi wetu umekua ukihitaji mageuzi kwa miongo kadhaa sasa. Mageuzi tuliyoweka yana lengo la kuimarisha msingi bora kwa ajili ya ukuaji wa siku za mbele” alisema rais huyo wa Nigeria.