Rais Bashir aahidi kurejesha amani jimbo la Kordofan

Waandamanaji wakitoa matamko ya kupinga serikali mjini Khartoum, Sudan, Jan. 24, 2019.

Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, Jumatatu ameahidi kurejesha amani katika jimbo la Kordofan Kusini ambako majeshi ya nchi hiyo yanapambana na waasi.

Wakati huohuo jeshi limeendelea kupambana na waandamanaji wakipanga maandamano dhidi ya serikali katika maeneo mbalimbali yenye mizozo nchini humo.

Rais Bashir amesema kuwa waandamanji wa Sudan wanajaribu kuiga wimbi la mapundizi ya kiarabu (Arab Spring) yalioshuhudiwa mwaka 2011 ambayo yalisababisha mageuzi makubwa.

Raia wa Sudan wamekuwa wakiandamana karibu kila siku tangu Disemba 19 wakimtaka rais ajiuzulu.

Bashir amekuwa anakabiliana na upinzani mkali zaidi tangu aliposhika hatamu za uongozi kwa njia ya mapinduzi mwaka 1989 .