Ndege hiyo iliipiga ndege ya Marekani na kuiharibu, jeshi la Marekani lilisema Jumanne, ikiwa ni tukio la karibuni katika mtiririko wa uchokozi wa Russia katika kuingilia kati droni za Marekani zinazoruka katika eneo hilo.
Kamanda mwandamizi wa Jeshi la Anga alisema hatua hiyo iliyotokea Jumapili ilikuwa ni jaribio la Russia kuiangusha droni ya Marekani aina ya MQ-9 Reaper kutoka angani na imekuja wiki tu baada ya ndege ya kivita ya Russia kuruka karibu ikihatarisha usalama wa ndege ya uchunguzi ya Marekani inayosafirisha wafanyakazi katika eneo, ikihatarisha maisha ya Wamarekani wanne waliokuwa ndani yake.
“Moja ya fataki zilizopigwa na Russia ziliigusa droni ya Marekani MQ-9, na kuharibu panga boi lake,” Lt. Jenerali Alex Grynkewich, mkuu wa Majeshi ya Anga ya Marekani Kati, alisema katika taarifa iliyo elezea wito wa hivi karibuni.
“Tunatoa wito kwa majeshi ya Russia huko Syria kuacha mara moja uzembe huu, unaofanywa bila ya uchokozi na tabia isiyokuwa na weledi.
Grynkewich alisema mmoja wa wafanyakazi wanaoendesha droni hizo ardhini aliiweka hewani na kuirusha kurejea katika kituo chake.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.