Majeshi ya Israeli yamerejea kuendeleza mapigano upande wa Ukanda wa Gaza

Moshi ukiwa umetanda kufuatia mashambulizi ya mabomu huko Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza Mei 12, 2024, huku vita kati ya Israel na Hamas vikiendelea.

Majeshi ya Israeli yamerejea kuendeleza mapigano upande wa kaskazini wa Ukanda wa Gaza.

Ndege ya kivita ya Israel ilishuhudiwa ikirusha fataki zenye kutoa mwanga wakati ikiruka katika eneo linalopakana na Jabalia huko kaskazini mwa Gaza Jumanne.


Mapigano mapya huko yamesisitiza wasiwasi nchini Israel kwamba ukosefu wa mpango wa mkakati wa wazi kwa Gaza utaiacha Hamas kuwa na udhibiti imara wa eneo finyu ambalo wamelitawala tangu mwaka 2007.


Ndege ya kivita ilionekana ikiruka kuvuka mpaka wa eneo linalopakana na Jabalia, huku helikopta ikiwa imetua karibu na eneo hilo muda mfupi baadae.


Mapigano makali yamefanyika kote upande wa kaskazini na kusini wa eneo la Palestina, huku vifaru vya Israeli vikiingia ndani kusini wa mji wa Rafah, ambako jeshi linasema kuna vikosi vinne vya mwisho vya Hamas vimejificha.

Vita kati ya Israel na Hamas vilianza baada ya shambulizi la Oktoba 7, ambapo Hamas walivishitukiza vikosi vya ulinzi mbalimbali vya Israel na kuvamia jamii kadhaa, wanamgambo hao wa Palestina waliwauwa watu 1,200, wengi wao raia.⁣