Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 01:53

Misaada ya kibinadamu inapungua Gaza; anasema Naibu msemaji wa UN


Wa-Palestina waliokoseshwa makaazi wakijiandaa kukimbia Rafah. May 13, 2024.
Wa-Palestina waliokoseshwa makaazi wakijiandaa kukimbia Rafah. May 13, 2024.

Bado hakuna usafirishaji wa bidhaa za kibinadamu zinazopitia kwenye kivuko cha Rafah ambacho kimefungwa, anasema Farhan Haq

Misaada ya kibinadamu inapungua Gaza wakati vivuko viwili vikuu karibu na Rafah, kusini mwa Gaza City, bado vimefungwa Jumatatu na wafanyakazi wa misaada walitaabika kusambaza vifaa vichache, pamoja na chakula kwa maelfu ya Wapalestina walioachwa bila makaazi.

Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari hapo Jumatatu kwamba usambazaji wa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo umesitishwa.

“Bado hakuna usafirishaji wa bidhaa za kibinadamu zinazopitia kwenye kivuko cha Rafah, ambacho kimefungwa”, alisema. “Na bado kuna ukosefu wa usalama na unaofaa kwa njia ya Kerem Shalom.

Tunajaribu kupata vitu, ikiwemo kupitia kivuko cha Erez, lakini kiasi cha vitu vinavyosafirishwa imekuwa kidogo sana katika siku za hivi karibuni”. Aliongeza “Katika hatua hii tunatoa mgao wa mafuta. Tumepungukiwa sana na mafuta.

Forum

XS
SM
MD
LG