Hata hivyo zaidi ya nusu ya mataifa yanayo shuhudhia kupunguka kwa maambukizo na vifo yameanza kufunguwa shughuli za biashara na kiuchumi polepole huko Ulaya.
Hata hivyo wataalmu wa kiuchumi wanatahadharisha juu ya uwezekano wa kuwepo ukosefu wa ajira kwa kipindi cha muda mfupi.
Wataalam hao wanaeleza kuwa hatari ya kweli inayoweza kuwa na athari mbaya zaidi kiuchumi ni pale ukosefu wa ajira utakapoendelea kwa muda mrefu.
Taarifa za kiuchumi zinaonyesha kuwa uchumi wa ufaransa umeingia katika hali ya kudumaa baada ya mapato ya robo ya kwanza kushuka kwa zaidi ya asilimia 6 tangu nchi hiyo iliposhuka kiuchumi mwaka 1945.
Kwa kila wiki mbili wakati nchi hiyo ikiwa inatekeleza amri ya kutotoka nje, Benki Kuu ya Ufaransa inatarajia uchumi kutetereka kwa asilimia 1.5.
Amri ya kutotoka nje iliyoanza kutekelezwa Machi 17 na imeongezwa kwa wiki mbili zaidi hadi Aprili 15, lakini mamlaka husika imesema huenda hali hii ikaendelea iwapo vírusi hivyo havionyeshi dalili ya kutoambukiza.
Kati ya sekta zilizoathirika vibaya zaidi katika uchumi, Benki ya Ufaransa iliorodhesha sekta hizo kama ujenzi, usafiri, migahawa na hoteli.
Wakati huohuo Uhispania, Itali, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza, Uholanzi, Uswitz hazikuripoti maambukizi mapya katika saa 24 zilizopita. Ubeljiji imeripoti visa vipya 660 pamoja na vifo 93 mnamo saa 24 zilizopita.
Russia imeripoti maambukizi mapya 7,099 na vifo 101.
Katika bara la Asia, China imeripoti visa vipya 4 katika saa 24 zilizopita.
Japan imeripoti maambukizi mapya 70 na vifo 12. Korea Kusini imeripoti visa vipya 4 pamoja na kifo kimoja.
Huko Mashariki ya Kati, Iran na Uturuki hazikuripoti visa vipya katika saa 24 zilizopita.
Amerika Kusini, Mexico zimeripoti maambukizi mapya elfu 1047 pamoja na vifo 163 mnamo saa 24 zilizopita.