Myanmar : Rufaa ya waandishi wa Reuters yakataliwa, warudishwa jela

Ndugu za waandishi wa habari wa Reuters waliofungwa wakiondoka mahakamani baada ya rufaa yao kukataliwa na mahakama ya kuu, Yangon, Myanmar, Januari 11, 2009.

Waandishi wawili wa habari nchini Myanmar rufani yao imekataliwa Ijumaa dhidi ya kosa walio hukimiwa kwalo na kifungo cha miaka saba jela.

“Ilikuwa ni adhabu stahili,” Jaji wa Mahakama ya Kuu Aung Naing ameeleza kuhusu hukumu hiyo.

Than Zaw Aung, ambaye ni wakili wa waandishi hao wa shirika la habari la Reuters amesema : Mahakama haikukubaliana na ukweli tulioueleza wakati wa rufani hiyo.

Kwa hiyo waliitupilia mbali rufani yetu na waandishi wataendelea kutumikia kifunga cha hadi miaka 7, sawa na uamuzi uliotolewa na mahakama huko siku za nyuma.

Rais wa Reuters na Mhariri Mtendaji Mkuu Stephen Adler amelaani “uonevu unaofanywa kwa wengi ulioelekezwa kwa waandishi Wa Lone na Kyaw Soe Oo.”

Adler amesema : “Waandishi hao ambao bado wako jela kwa sababu moja tu: wale waliooko madarakani wanalazimisha kuzima ukweli. Kuripoti siyo kosa la jinai, na mpaka pale Myanmar itakapo rekebisha jambo hili ambalo siyo sahihi kabisa, vyombo vya habari Myanmar havitakuwa huru, na ahadi ya Myanmar kuheshimu utawala wa sheria na demokrasia utakuwa unaleta shaka.”

Wakijibu uamuzi huo nje ya mahakama balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Myanmar Kristian Schmidt amesema alikuwa anategemea rais wa Myanmar “kusahihisha” dhulma hiyo kwa kutoa msamaha.

“Hivi sasa tunahisi kuwa ni juu ya Rais wa Myanmar kusahihisha dhulma hiyo iliyo fanyika na Umoja wa Ulaya tunarejea kauli yetu kwamba waandishi hawa waachiwe huru mara moja na bila masharti.”

Wa Lone na Kyaw Soe Oo walikamatwa Disemba 2017 kwa makosa ya kuvunja sheria ya siri za serikali za nchi ya Myanmar.

Jaji wa mahakama hiyo ambaye aliendeleza hukumu iliyotolewa amesema mawakili wa waandishi hao hawakuweza kutoa ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa hawana makosa.

Waandishi hao wanasema walikamatwa katika mpango uliokuwa umetengenezwa na polisi ili kuzuia habari za mauaji ya Rohingya zisiandikwe, ambao ni kikundi cha walio wachache cha Waislam nchini Myanmar.

Umoja wa Mataifa umefananisha mashambulizi ya kikatili yaliyo fanywa na jeshi la Myanmar kwa watu wa kabila la Rohingya ni mauaji ya halaiki.