Mtuhumiwa alikwenda katika jengo la chuo, Jumatatu asubuhi na kuanza kufyatua risasi.
Wanafunzi na waalimu walijificha ndani ya jengo la chuo wengine walionekana wakiruka kutoka kwenye madirisha.
Polisi wamesema walimjeruhi na kumkamata mshambuliaji ambaye inasemekana kuwa ni mwanafunzi.
Zaidi ya watu 20 wamejeruhiwa katika tukio hilo. Kulikuwa na takriban watu 60 ndani ya darasa.
“Tulifunga mlango na kujikinga na viti, mwanafunzi semyon karyakin ameliambia shirika la habari Reuters.”
Hata hivyo vyombo vya habari vimemtaja mshambuliaji kuwa ni mwanafunzi mwenye umri wa miaka 18 ambaye mapema alibandika picha yake katika mtandao wa kijamii akiwa na bunduki, kofia ya kujikinga na silaha.
“Nimefikiria hili kwa muda mrefu, imekuwa ni miaka mingi na nimegundia muda umefika wa kufanya kitu nilichokuwa nakifikiria, alisema katika mtandao wa kijamii ambapo baadae akaunti yake ilifutwa.
Alisema kuwa hatua zake hazihusiani na siasa wala dini lakini zilichochewa na chuki.