Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 14:16

Paul Rusesabagina akutwa na hatia ya kufadhili ugaidi


Paul Rusesabagina akiwa katika mahakama kuu mjini Kigali February 17, 2021 wakati wa kesi kusikilizwa kesi yake.
Paul Rusesabagina akiwa katika mahakama kuu mjini Kigali February 17, 2021 wakati wa kesi kusikilizwa kesi yake.

Paul Rusesabagina, shujaa wa Hoteli ya Rwanda ambaye alikua mkosoaji mkali wa serikali, alipatikana na hatia siku ya Jumatatu kwa mashtaka ya ugaidi.

Paul Rusesabagina, shujaa wa Hoteli ya Rwanda ambaye alikua mkosoaji mkali wa serikali, alipatikana na hatia siku ya Jumatatu kwa mashtaka ya ugaidi baada ya kile wafuasi wake wanasema ilikuwa kesi yenye ushawshi wa kisiasa.

Alikutwa na hatia kwa kuunga mkono kundi la waasi wanaolaumiwa kwa shambulio baya la bunduki, guruneti na uchomaji moto nchini Rwanda mnamo 2018 na 2019.

Alianzisha taasisi ya kigaidi ambayo ilishambulia Rwanda, alichangia kifedha katika shughuli za kigaidi," Jaji Beatrice Mukamurenzi alisema mwishoni mwa kesi hiyo ya miezi saba.

Waendesha mashtaka wa Rwanda wameomba kifungo cha maisha jela kwa Rusesabagina, mfanyakazi wa zamani wa hoteli mwenye umri wa miaka 67 anayesifiwa kuokoa mamia ya watu wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994, na ambaye matendo yake yalipelekea kutengenezwa kwa filamu ya Hollywood.

Si yeye wala mawakili wake walioruhusiwa kortini kwa uamuzi huo, ingawa washtakiwa wengine 20 katika kesi hiyo walihudhuria.

Rusesabagina, ambaye alitumia umaarufu wake kumshutumu kiongozi wa Rwanda Paul Kagame kuwa dikteta, alikamatwa mwezi Agosti 2020 wakati ndege ambayo aliamini ilikuwa ikielekea Burundi badala yake ilikwenda katika mji mkuu wa Rwanda Kigali.

Familia yake inasema Rusesabagina alitekwa nyara na alikuwa amekana mashtaka tisa dhidi yake kama ulipizaji kisasi wa serikali kwa maoni yake ya wazi.

Mapema mwezi huu, Kagame alikuwa amepuuza ukosoaji wa kesi hiyo, akisema Rusesabagina alikuwa kizimbani sio kwa sababu ya umaarufu wake lakini ni juu ya maisha yaliyopotea kwa sababu ya matendo yake.

XS
SM
MD
LG