Vyanzo vya habari vinasema hali ya mabadiliko hayo tayari yamemfanya mshirika wa al Qaeda kuwa na fursa zaidi kufanya operesheni zake.
Tangu rais Joe Biden alipochukua madaraka Januari 20, Marekani haijafanya shambulizi hata moja la anga dhidi ya al-Shabaab nchini Somalia, baada ya kufanya mashambulizi saba kuanzia Januari 1 hadi 19.
Maafisa waandamizi wa jeshi la Somalia wana wasi wasi kuwa muongozo mpya, ambao umewekwa kuimarisha udhibiti katika utaratibu wa kuamuru mashambulizi na unahitaji idhini ya White House kwa operesheni, una maana kuwa al-Shabaab itaanza kukusanya nguvu tena.
Maafisa wa ulinzi na upelelezi wa Marekani kwa muda mrefu umeliona kundi la al-Shabaab lenye makao yake Somalia ni tishio kubwa huko Afrika.