Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 18:56

Uhuru akutana na rais wa Somaliland Muse Bihi wakati mzozo kati ya Kenya na Somalia unaendelea


Rais wa Somaliland Muse Bihi Abdi
Rais wa Somaliland Muse Bihi Abdi

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amefanya mazungumzo na rais wa Somaliland Muse Bihi, wakati uhusiano kati ya Kenya na Somalia ukionekana kuyumba yumba.

Somalia ilimfukuza balozi wa Kenya mjini Mogadishu mwezi uliopita, na kuamurisha balozi wake mjini Nairobi kurudi Somalia.

Serikali ya Somalia inadai kwamba Kenya inaingilia mambo yake ya ndani, Pamoja na siasa zake.

Wizara ya mambo ya nje ya Kenya imesema kwamba mazungumzo kati ya Kenyatta na Bihi, yataangazia maslahi ya nchi hizo mbili.

Ujumbe wa twiter wa wizara hiyo umesema kwamba Somaliland ni muhimu sana katika ushirikiano wa nchi za pembe ya Afrika katika kupambana na ugaidi hasa kundi la kigaidi la Al-shabaab.

Hii ni mara ya pili kiongozi wa Somaliland anatembelea Kenya. Mara ya kwanza ilikuwa ziara ya rais Kahin Riyale Kahin, mwaka 2006.

Somaliland ilijitangazia uhuru mwaka 1991 lakini uhuru huo haujatambuliwa na umoja wa mataifa wala Umoja wa nchi za Afrika au nchi yoyote.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG