Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:28

Upinzani Somalia unakataa kumtambua Farmajo kama Rais halali nchini humo


Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo

Rais Mohamed Abdullahi Farmajo muhula wake wa miaka minne madarakani umemalizika Februari 8 na muungano wa wagombea urais wa upinzani kupitia msemaji wao Ridwan Hajji wamesema hawatamtambua Farmajo kama mkuu wa nchi

Wanachama wa vyama vya upinzani Somalia wameapa kutomtambua kabisa Mohamed Abdullahi Farmajo kama rais wa nchi hiyo kufuatia kumalizika rasmi kwa muhula wake madarakani siku ya Jumatatu. Somalia bado imekwama katika matatizo ya kisiasa wakati uchaguzi umecheleweshwa na vyama vya siasa vimeshindwa kukubaliana jinsi ya kusonga mbele.

Washirika wa kimataifa wa Somalia, ikiwemo Marekani wanaonesha wasi wasi kuhusu mkwamo wa kisiasa ambao umechelewesha uchaguzi wa rais na wabunge nchini humo.

Rais Mohamed Abdullahi Farmajo, muhula wake wa miaka minne madarakani umemalizika Februari 8, na muungano wa wagombea urais wa upinzani kupitia msemaji wao Ridwan Hajji, wamesema hawatamtambua Farmajo kama mkuu wa nchi.

“Mohamed Abdullahi Farmajo lazima aheshimu katiba na kuachia majukumu yake kama mkuu wan chi. Tunatoa wito kwa wadau wote au washiriki katika utaratibu wa kisiasa kuunda baraza la mpito ambalo linajumuisha marais wa bunge la watu”.

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo

Hata hivyo, baadhi ya wabunge wengine kama Abdi Shire wanaamini Farmajo bado ni rais halali hadi atakapopatikana rais mwingine au kama atachaguliwa tena, kulingana na azimio lililoidhinishwa na mabaraza mawili ya bunge mwaka jana.

“Maazimio yaliopo ambayo yalipitishwa na bunge la taifa yanasema kwamba kama uchaguzi hautafanyika kwa wakati uliowekwa, wote wanaoshikilia ofisi kikatiba pamoja na Rais watakuwa madarakani hadi watakapopata warithi wao kupitia uchaguzi”

Somalia ilipanga kufanya uchaguzi usio wa moja kwa moja wa bunge mwishoni mwa mwaka jana, kabla ya uchaguzi wa rais mwezi Februari.Lakini mchakato huo umekwama kutokana na kutokubaliana kati ya wadau wa kisiasa juu ya nani atakayehudumu kwenye tume inayosimamia uchaguzi huo.

Profesa Afyare Elmi ni profesa msaidizi wa masuala ya usalama katika chuo kikuu cha Qatar. Anasema kama pande zote mbili hazikubaliani katika mtazamo wenye manufaa kwa taifa, kunaweza kuwa na vikwazo vya usalama nchini Somalia katika wiki zijazo.

Siku ya Jumapili, wanachama 12 wa vikosi vya usalama Somalia waliuwawa katika mlipuko uliotokea karibu na mji wa Dhusamareb. Wanamgambo wa al-Shabaab walidai kuhusika.“Madhara ya usalama yanaweza kuwa tatizo ikiwa hakuna suluhisho katika wiki chache zijazo kwa sababu kuna ubaguzi ndani ya tabaka la kisiasa na kwa miaka minne iliyopita, rais na utawala wake hawakusaidia katika kudhibiti utofauti wa makundi ya kisiasa Somalia.”

Rais Farmajo hakutoa maoni Jumatatu lakini Jumamosi alilihutubia bunge, akisema utawala wake utajaribu kutekeleza makubaliano ya Septemba juu ya kufanya uchaguzi. Hiyo inamaanisha ataendelea kuwepo madarakani hadi vyama vitakapokubaliana juu ya njia muafaka ya kumchagua mrithi wake.

XS
SM
MD
LG