Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:44

Rais wa Somalia hatakiwi kushiriki mazungumzo yeyote ya kutatua mzozo nchini humo


Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed maarufu Farmajo
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed maarufu Farmajo

Muhula wake kuwepo madarakani uliisha mwanzoni mwa Februari na bunge lilipanga kufanya uchaguzi Februari 8 ukacheleweshwa kwa sababu wabunge wapya bado hawajachaguliwa huku upinzani unamshutumu Farmajo kujaza wafuasi wake katika bodi ambazo huchagua wabunge

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed maarufu Farmajo ambaye muhula wake wa miaka minne madarakani ulifikia kikomo mwanzoni mwa mwezi huu hatakiwi kushiriki katika mazungumzo yanayolenga kutatua mzozo ambao umechelewesha kufanyika uchaguzi mkuu mpya wa nchi hiyo, serikali za majimbo mawili kati ya matano nchini Somalia zimesema Jumapili.

Bunge lilipanga kufanya uchaguzi Februari 8 lakini uchaguzi ukacheleweshwa kwa sababu wabunge wapya bado hawajachaguliwa huku wapinzani wa Rais Mohamed Abdullahi Mohamed ambaye anawania muhula wa pili madarakani, wanamshutumu kujaza wafuasi wake kwenye bodi za mkoa na kitaifa ambazo huchagua wabunge.

Wafuasi wa vyama tofauti vya upinzani wakiandamana kufuatia ucheleweshwaji wa uchaguzi
Wafuasi wa vyama tofauti vya upinzani wakiandamana kufuatia ucheleweshwaji wa uchaguzi

Ucheleweshaji huo umezidisha mivutano katika taifa hilo la pembe ya Afrika ambalo liliharibiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na ambalo bado linapambana na uasi unaofanywa na kundi la kiislam la al-Shabaab ambalo mara kwa mara linafanya mashambulizi mjini Mogadishu na kwingineko.

Serikali ya Jubaland, moja ya mikoa mitano ya Somalia imesema kipindi cha Rais Mohamed Abdullahi Mohamed kuwepo madarakani kimeisha na anapaswa kujitoa katika mazungumzo yeyote juu ya mzozo huu.

XS
SM
MD
LG