Martin Fayulu, tajiri wa zamani wa biashara ya mafuta, anasema serikali lazima itangaze matokeo ili kuepusha mivutano zaidi.
Mgombea urais wa upinzani Martin Fayulu amewaonya maafisa wa uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo “kutoficha ukweli” wakati mvutano unaendelea kufukuta juu ya kucheleweshwa kwa matokeo ya uchaguzi.
Fayulu amesema “Wananchi wa Congo tayari wanajua” matokeo ya kura hizo, zilizo pigwa Disemba 30.
Matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa hapo awali yanategemewa kutangazwa Jumapili.
Uchaguzi huo utawezesha kupatikana mtu atakaye chukuwa nafasi ya urais inayoachwa na Joseph Kabila baada ya kutangaza kutoendelea na uongozi ambaye amaeachia madaraka baada ya kutumikia nafasi ya urais kwa miaka 18..