Mkuu wa haki za binadamu UN awataka majenerali wa Sudan kusitisha 'ghasia zisizokuwa na maana'

FILE PHOTO: Mtu akitembea wakati moshi ukitanda juu ya majengo baada ya shambulizi la angani Khartoum Kaskazini.

Mkuu wa masuala ya haki za binadamu katika  Umoja wa Mataifa ameelezea hali ilivyo nchini Sudan  kuwa inavunja moyo sana na ametoa wito  wa moja kwa moja kwa majenerali wawili wanaogombana kusitisha  manyanyaso ya ngono na kuokoa maisha ya raia.

Mapigano nchini Sudan ambayo yalizuka zaidi ya mwezi mmoja uliopita yamesababisha vifo vya mamia ya raia na kuwalazimisha zaidi ya milioni wengine kukimbia ghasia hizo.

Voker Turk ambaye amekutana na majenerali wote wawili nchini Sudan mwezi Novemba amesema ofisi yake imepokea ripoti ya ndege za kivita na mapambano katika mji mkuu wa Khartoum usiku kucha licha ya kuwepo sitisho la mapigano.

Amesema ofisi yake imerekodi takriban kesi 25 za manyanyaso ya ngono hadi sasa, na kwamba idadi halisi inaweza kuwa kubwa zaidi.

Kamishna mkuu wa umoja wa mataifa wa masuala ya haki za binadamu, Volker Turk anaeleza:“ Inavunja moyo kile kinachotokea nchini Sudan. Licha ya kuwepo sitisho la mapigano yaliyofanya kazi na bado wanaendelea kufanya mipango hii, tunaona kwamba wanaendelea kuzungumzia hayo ndani ya saa kadhaa baada ya makubaliano haya kutiwa saini. Tunaona jinsi raia wanavyoendelea kukabiliwa na hatari kubwa ya kifo na majeraha. Ninamaanisha, usiku tulipokea ripoti za ndege za kivita kuwepo kote Khartoum na mapigano katika baadhi ya maeneo ya jiji , pamoja na milio ya risasi iliyosikika Khartoum kaskazini, na Omdurman.

Sitisho la mapigano ambalo linafuatiliwa na Saudi arabia na marekani pamoja na pande zinazogombana linakuja baada ya wiki tano za mapigano makali katika mji mkuu wa Khartoum na ghasia nyingine katika baadhi ya maeneo ya nchi ikiwemo mkoa wa magharibi wa Darfur.