Mkutano wa COP29 waanza Azerbaijan

Mwanamazingira Greta Thunberg ashirki katika mgomo huko Georgia Novemba 11, 2024. Picha na REUTERS/Irakli Gedenidz

Mkutano wa mwaka wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa COP29 umeanza Jumatatu wakati nchi zikijitayarisha kwa mazungumzo magumu kuhusu fedha na biashara, kufuatia mwaka mzima wa majanga ya hali ya hewa

Majanga ambayo yamezipa ujasiri nchi zinazoendelea katika madai ya fedha za kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Rais anayeondoka madarakani wa COP29 Sultan Al- Jaber alifungua Mkutano huo na kukabidhi urais kwa Mukhtar Babayev wa Azebaijan, ambaye aliwaambia washiriki kwamba mkutano huo utakuwa ni wakati wa ukweli kwa makubaliano ya Paris.

Wajumbe wanakutana Baku, wakiwa na matarajio ya kutatua ajenda ya juu ya COP29, mpango wa karibu dola trilioni 1 kwa ajili ya fedha za hali ya hewa kwa nchi zinazoendelea, ikiziba nafasi ya lengo la dola bilioni 100.

Lakini lengo la ufadhili ni kushindana kwa umakini katika wasiwasi wa kiuchumi , vita vya ukraine na Gaza na kuchaguliwa kwa Donald Trump kwa muhula wa pili kuwa rais wa Marekani katika taifa lenye Uchumi mkubwa zaidi duniani, ambaye anaonekana kuwa mkaidi wa mabadiliko ya hali ya hewa.