Kongamano hilo linalohudhuliwa na takriban wajumbe 5,000 wakiwemo wakulima, wakuu wa serikali mbalimbali wabunifu na wasomi kujadili mikakati ya kukomesha njaa kwa takriban watu milioni 20 wanaokabiliwa na baa la njaa barani Afrika na kuwawezesha kunapata lishe.
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo kutoka Tanzania Joleta Joseph amesema kuwa, “Tofauti ya zamani na sasa ni kwamba zamani unakuta kila kitu kilikuwa ni kwa mkono lakini kinachozalishwa kinakuwa ni kidogo sanaa, ikiwa ni kwneye chakula lakini pia kwenye usindikazi kila sehemu lakini ukiangalia sasa kwenye matumizi ya teknologia tunazalisha mwaka mzima kwamba tunatumia teknologia za umwangiliaji manake utazalisha kipindi chote cha mwaka kwa hiyo manake tuna uhakika wa mali ghafi,”
“lakini tukija kwenye usindikazi unaweza kusindika mwaka kwa kiwango kikubwakwa kutumia teknologia lakini pia utakuw aumelinda ubora wa kile ambacho ukizalisha” aliongeza.
Licha ya kuzalisha aina mbalimbali ya chakula bara la Afrika bado linaagiza chakula kutoka nje, washiriki wanasema changamoto hii inaweza kutatuliwa kwa kutumia teknolojia ya kilimo.
Mshiriki huyo kutoka Tanzania pia amesema, “Teknologia kwa sasa hivi ni kila kitu cha kwanza kinasahirisha upatikani wa chakula lakini pia uzalishaji pili kinatoa ubora wa kile ambacho tunachokizalisha, kwa mfano tunaongelea teknologia za ukaushaji mimi ni msindikaji nakausha vizilishe natumia solar teknomimi,” amesema.
Ni kauli inayoungwa mkono na Fatuma Mang’enya kutoka Tanzania, yeye ni mwanzilishi wa kampuni inayosarifu mwani kwa kuongeza thamani kwa kutengeneza bidhaa za chakula.
Naye Fatuma Mang’enya Mshiriki kutoka Tanzania amesema.
“Tukiangalia kwenye upande wa kuongeza thamani tumewaonyesha jinsi ya kutumia teknologia tofauti jinsi ya kuongeza thamni katika hili zao la thamani”
Mabadiliko ya hali ya hewa yanazidi kuathiri mbegu zinazotumika katika upandaji wa mavuno barani Afrika, ili kutatua matatizo.
Tony Gathungu mtafiti wa mbegu kutoka Kenya anasema kujumulsha utafiti katika kilimo kutasaidia sio tu kuimarisha kilimo bali pia kuhakikisha mimea inaweza kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Gathughu amesema. “Kuna teknologia ambayo watu hawajaifahamu sana ambayo ni gmo na hiyo ni teknologhia ambayo inawawezesha wakulima kuzalisha mbegu bila ya kutumia dawa”
Mbona usichukue mbegu za kisasa mbegu za kisasa ndizo zitakazokuwezesha kupata manufaa kwa sababu changamoto zipo hali ya hewa ndio hiyo na haijulikani,Kama kenya sasa mvua inafaa ianze kunyesha sasa hivi haijanyesha inafaa kunyesha mwenzi wa tatu inakuja mwezi wa tano kwa hivyo unataka mbegu ambazo zinaweza kumea kwa wakati mdogo sana” ameongeza.
Lakini huenda maono haya yakakosa kufanikiwa kikamilifu kama kiwango cha fedha zinazoelekezwa katika kilimo barani Afrika kitaendelea kuwa chini, na sasa changamoto imetolewa kwa serikali barani humu kuimarisha kiwango kinachotengwa kwa kilimo kutoka asilimia nne ya sasa hadi kumi.
Profesa Hamad Boga ambaye ni naibu rais wa shirika la AGRA amesema
“Asilimia 85 ya biashara ya chakula inayotendeka afrika watu ambao ni wawekezaji binafsi na maranyingi huwa hawahitaji mambo mengi inayotendeka seriklai itekeleze majukumu yake ya kimsingi ambapo ni kuhakikisha kwamba kuna Barabara, masoko kuna kawi kuna vitu kamainternet na ict kuna maji wao wakiona mazingira ni mazuri tayari watawekeza na hiyo sekta itapanuka.”
Pia amesema kuwa “Afrika inaweza kujilisha asilimia 85 ya chakula kinacholiwa Afrika kinatoka Afrika ni aslimia kidogo tu ambayo inaletwa kutoka nje’."
Katika mkutano huo pia imebainika mmoja kati ya watu watano barani Afrika wanakabiliwa na njaa, hii ikiwa ni kinyume na makubaliano ya Malabo nchini Equitorial Guinea mwaka 2014 ambapo viongozi katika mkutano wa umoja wa Afrika walikubaliana kumaliza janga la njaa Barani Afrika kufikia mwaka 2025.
Imetayarishwa na Zainab Said, Sauti ya Amerika Nairobi, Kenya
Forum