Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:53

Nchi za Afrika zapoteza mapato kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.


Watu wamekusanyika kufanya tathimini ya uhalibifu katika mtaa uliojaa matope kutokana na maporomoko ya aridhi na mafuriko huko Tanzania. Picha na Ebby SHABAN / AFP
Watu wamekusanyika kufanya tathimini ya uhalibifu katika mtaa uliojaa matope kutokana na maporomoko ya aridhi na mafuriko huko Tanzania. Picha na Ebby SHABAN / AFP

Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) limesema Mataifa ya Afrika yinapoteza hadi asilimia tano ya Pato la Uzalishaji wa Kitaifa (GDP) kila mwaka kutokana na kubeba mzigo mkubwa zaidi kuliko dunia nzima kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Katika ripoti yake mpya WMO ilisema Jumatatu kwamba baada mfululizo wa miaka yenye joto zaidi barani Afrika kuwahi kutokea, nchi nyingi za Afrika zinatumia hadi asilimia tisa ya bajeti zao kwa ajili ya kutekeleza sera za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

“Kwa kipindi cha miaka 60 iliyopita, Afrika imeshuhudia mwenedo wa ongezeko la joto ambalo limekuwa la kasi zaidi kuliko wastani wa dunia,” alisema Katibu Mkuu wa WMO, Celeste Saulo, akionya kwamba inaathiri kila kitu kutoka usalama wa chakula hadi afya ya umma na amani.

Afrika inachangia chini ya asilimia kumi ya uzalishaji wa gesi chafu duniani. Lakini ni kanda iliyoko hatarini zaidi kwa matukio mabaya ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na ukame, mafuriko na mawimbi ya joto, imesema WMO.

Ripoti mpya inazingatia mwaka wa 2023, moja ya miaka mitatu iliyokua joto kali zaidi kuwahi kutokea barani Afrika.

Ripoti hiyo ilihimiza serikali za Afrika kuwekeza katika mifumo ya tahadhari ya mapema pamoja na huduma za hali ya hewa. Iwapo hatua za kutosha hazitachukuliwa, Waafrika milioni 118 wataathirika na ukame, mafuriko na joto kali ifikapo mwaka 2030, ripoti ilionya.

Nyumba zikiwa zimefurika maji katika wilaya ya Rufij, Tanzania Aprili 25, 2024.
Nyumba zikiwa zimefurika maji katika wilaya ya Rufij, Tanzania Aprili 25, 2024.

Katika nchi za Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara, gharama za kukabiliana na hali ya hewa mbaya zinaweza kufikia dola bilioni 30-50 kwa mwaka katika muongo mmoja ujao, ripoti ilikadiria.

Madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa yamekuwa ya kutisha. Kati ya Septemba na Oktoba 2023, takriban watu 300,000 Afrika Magharibi waliathiriwa na mafuriko, ripoti ilisema. Zambia ilikumbwa na ukame mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 40, na kuathiri karibu watu milioni 6.

Mwenendo wa matukio ya hali ya hewa kali barani Afrika utaendelea kwa mwaka 2024, wataalamu walisema.

Katika kanda ya Sahel, kusini mwa Sahara, mafuriko yameathiri zaidi ya watu 716,000 mwaka huu, kulingana na Umoja wa Mataifa. Nchini Mali, maafisa wiki iliyopita walitangaza janga la kitaifa kutokana na mafuriko yaliyowaathiri zaidi ya watu 47,000 tangu mwanzo wa msimu wa mvua.

Afrika Magharibi ilikumbwa na wimbi la joto lisilo la kawaida mapema mwaka huu ambalo limesababisha ongezeko la vifo.

Forum

XS
SM
MD
LG