Taarifa zinaeleza mwanzilishi huyo wa Kanisa liitwalo Sinagogi ya Mataifa Yote, alifariki saa 2 asubuhi leo Jumapili, saa kadhaa baada ya kuacha ibada ikiendelea, kwenye kanisa lake kuu mjini Lagos, na kwenda nyumbani kwake kupumzika.
Ripoti zinasema Joshua alitoka kanisani kwenda nyumbani kwake, alipojisikia vibaya wakati wa ibada hiyo iliyoanza mwendo wa saa kumi na mbili jioni, jana Jumamosi.
Baada ya kupatwa na wasiwasi kuhusu kiongozi wao, wasaidizi wake walikwenda kumuangalia nyumbani kwake, lakini wakakuta amekufa, shirika la habari la CNN limeripoti.
Sababu ya kifo cha Joshua, aliyeanza kupata umaarufu miaka ya tisini, akidai kuwaponya waumini kwa miujiza, haikuwa imeelezwa hadi tulipokuwa tukienda mitamboni.