Gavana wa jimbo hilo la Colorado Jered Polis alisema ametiwa moyo na wasifu wa kuvutia wa Mobolade.
"Mtu ambaye amejitolea maisha yake na kuifanya Colorado Springs na Amerika kuwa mahali pazuri zaidi, mwenye historia ambayo wote tunaweza kuielewa, amekuja hapa, na kuanzisha biashara.” Alisema Polis wakati wa sherehe ya kuapishwa kwake.
Mobolade alihamia Marekani miaka 27 iliyopita akiwa mwanafunzi na akawa raia wa Marekani mwaka wa 2017. Alianza familia, akafungua migahawa miwili na kanisa, kisha akashinda uchaguzi katika jiji hili la kihafidhina akiwa kiongozi wa kwanza mweusi kuchaguliwa katika jiji hilo.
"Ninapoamka kila asubuhi ninadhani nipo ndotoni, halafu nagundua, hapana, jambo hili ilitokea kweli," Mobolade alisema.
Lakini kilichomfanya aaminiwe na wakazi wengi, baadhi yao walisema, ni wakati ule alipokuwa meneja wa maendeleo ya biashara ndogo ndogo mjini Colorado Springs kuanzia mwaka 2019 hadi 2022.
Baadhi ya wakazi waliiambia VOA kuwa ushindi wa Mobolade katika uchaguzi unatuma ujumbe kwamba jimbo lao linakaribisha watu kutoka matabaka yote ya maisha.
Mji wa of Colorado Springs, wenye takriban wakazi 500,000 ambapo zaidi ya asilimia 75 ni Wazungu, na waliona kuna matumaini kwa vile kulikuwepo na wapiga kura wengi walikua tayari kumuunga mkono mtu mwenye asili tofauti.