Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 05:31

Wapiganaji wa Boko Haram wamewateka nyara wafugaji 30 huko Nigeria


Mfano wa wanamgambo wa Boko Haram huko nchini Nigeria
Mfano wa wanamgambo wa Boko Haram huko nchini Nigeria

Wanamgambo hao wakiwa katika boti nane walivamia vijiji vya wavuvi na wafugaji huko Tudun Kwastan, Kwatar Turare na Kwatar Kuwait katika mwambao wa ziwa hilo siku ya Ijumaa na kuwateka wafugaji 30 wakiwemo wanaume na wanawake, vyanzo hivyo vimesema

Wapiganaji wa Boko Haram wamewateka nyara wafugaji 30 wa kabila la Fulani karibu na Ziwa Chad kaskazini mashariki mwa Nigeria, wakidai fidia ili waachiliwe, wavuvi na mkuu wa kundi linalowapinga wanamgambo wa itikadi kali za kislamu waliliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumanne.

Wanamgambo hao wakiwa katika boti nane walivamia vijiji vya wavuvi na wafugaji huko Tudun Kwastan, Kwatar Turare na Kwatar Kuwait katika mwambao wa ziwa hilo siku ya Ijumaa, na kuwateka wafugaji 30, wakiwemo wanaume na wanawake, vyanzo hivyo vimesema.

Wapiganaji wa Boko Haram walikwenda na kuchagua nyumba za kabila la Fulani katika vijiji hivyo na kuwachukua wanaume na wanawake 30, Labo Sani, mvuvi kutoka eneo jirani la Doron Baga, aliliambia shirika la habari la AFP.

Waliacha ujumbe wakizitaka familia za mateka hao kuchangisha naira milioni 20 sawa na dola 43,000 kwa ajili ya kuachiliwa kwa familia hizo, Labo alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG