Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:07

Boko Haram waua watu 12 Cameroon


Kikosi cha Rapid Intervention Force kikifanya doria katika eneo linalo shikiliwa na Boko Haram la Mosogo huko Cameroon, Machi 21 2019. Picha na Reinnier KAZE / AFP.
Kikosi cha Rapid Intervention Force kikifanya doria katika eneo linalo shikiliwa na Boko Haram la Mosogo huko Cameroon, Machi 21 2019. Picha na Reinnier KAZE / AFP.

Maafisa kaskazini mwa Cameroon wamefanya mkutano wa dharura siku ya Jumatano wakiziomba nchi za Cameroon, Nigeria na Chad kupeleka wanajeshi zaidi katika mpaka wanaoshirikiana, baada ya mashambulizi mapya ya Boko Haran ambayo yameua watu takriban 12 wakiwemo wanajeshi sita siku ya Jumanne.

Maafisa hao wanasema mamia ya wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu na wenye silaha nzito wamejiingiza katika eneo hilo tete la Ziwa Chad na kushambulia, kupora na kusababisha hofu.

Maafisa wa Jeshi na serikali katika taifa hilo la Afrika ya kati upande wa kaskazini mwa mpaka na Nigeria wanasema walifanya mkutano huo wa dharura siku ya Jumatano, chini ya saa 24 baada ya wimbi jipya la mashambulizi ya Boko Haram kuripotiwa.

Midjiyawa Bakari gavana wa jimbo la Far North nchini Cameroon ambalo linapakana na Chad na Nigeria, alizungumza na kituo cha utangazaji kinachomilikiwa na serikali ya Cameroon CRTV siku ya Jumatano.

Bakari alisema Rais wa Cameroon Paul Biya aliamuru maafisa na wanajeshi katika mkoa huo wa Far North kufanya mkutano wa dharura na kuhakikisha wanamgambo wa Kiislamu wenye silaha waliopenya katika eneo tete la Ziwa Chad wanazuiliwa.

Alisema Biya aliamuru kufanyika kwa mkutano huo wa dharura baada ya mamia ya wanamgambo kuwaua wanajeshi watatu, maafisa wawili wa forodha na raia wawili katika mashambulizi la kushtukiza dhidi ya wanajeshi wa serikali ya Cameroon walioko katika miji ya kaskazini ya Mora na Zigague siku ya Jumanne.

Gavana huyo alisema Boko Haram imedhoofika lakini bado inafanya mashambulia mengi katika jamii kwa lengo la kuwaua wapinzani wao na kuiba ng'ombe, chakula na fedha.

Forum

XS
SM
MD
LG