Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 05:43

Wasichana wa Chibok wameachiliwa huru na Boko Haram, wamezaa watoto


Wasichana waliokuwa wametekwa nyara na Boko Haram baada ya kuachiliwa huru
Wasichana waliokuwa wametekwa nyara na Boko Haram baada ya kuachiliwa huru

Wanawake wawili waliotekwa nyera nchini Nigeria na kundi la wanamgambo la Boko Haram, miaka tisa iliyopita wakiwa Watoto wa shule, wameokolewa na kurudi nyumbani wakiwa na Watoto wachanga.

Jeshi la Nigeria limetoa taarifa hiyo.

Mmoja wao ana mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na mwingine amejifungua mtoto wake wa pili siku chache baada ya kuokolewa huru.

Hauwa Maltha na Esther Marcus waalikuwa miongoni mwa wasichana wa shule 276 waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram, mnamo mwezi April mwaka 2014, kutoka shule ya upili ya wasichana inayomilikiwa na serikali, katika Kijiji cha Chibok.

Wanafunzi walikuwa wanajitayarisha kufanya mtihani wakati walipotekwa nyara.

Kamanda wa jeshi la Nigeria linalofanya msako dhidi ya Boko Haram Meja Jenerali Ibrahim Ali, amesema kwamba wanawake hao waliokolewa mnamo mwezi April na tayari wameungana na familia zao.

XS
SM
MD
LG