Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:15

Wafuasi 1,400 wa Boko Haram nchini Nigeria wamenaswa wakielekea Niger


Ramani ya Nigeria na maeneo jirani na nchi hiyo
Ramani ya Nigeria na maeneo jirani na nchi hiyo

Kuhama kwa kundi hilo kuelekea kusini mashariki mwa Niger kulianza mwezi machi wakati kundi la Islamic State West Africa Province (ISWAP) lilipowafuata Boko haram katika maficho yake kwenye msitu wa Sambisa huko kaskazini-mashariki mwa Niger

Takribani wafuasi 1,400 wa kundi la wanajihadi wa Boko Haram nchini Nigeria wamenaswa wakikimbilia Niger kufuatia mapigano na kundi hasimu la Islamic State kulingana na jeshi la Nigeria.

Kuhama kwa kundi hilo kuelekea kusini mashariki mwa Niger kulianza mwezi machi wakati kundi la Islamic State West Africa Province (ISWAP) lilipowafuata Boko haram katika maficho yake kwenye msitu wa Sambisa huko kaskazini-mashariki mwa Niger.

Vikosi vya jeshi la Niger hadi hivi sasa vimewachukua watu 1,397 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto kulingana na taarifa kutoka eneo la kusini-mashariki mwa jeshi ambazo zimeonekana kwa shirika la habari la AFP.

Watu hao wamekabidhiwa kwa mamlaka ya kijeshi ya Nigeria, taarifa ilieleza.

Takribani magaidi 30 waliokataa kujisalimisha waliuawa, iliongeza taarifa.

Kundi la Boko haram lilianzisha kampeni ya umwagaji damu huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria hapo mwaka 2009 ambayo ilisababisha vifo vya watu 4,000 na kuwakosesha makazi takribani watu milioni mbili, kulingana na takwimu za Umoja wa mataifa (UN).

Lilianza kujulikana duniani kote mwaka 2014 kwa kuwateka nyara wasichana 276 wa shule ya sekondari katika mji wa Chibok ambapo wasichana 96 kati yao bado hawajulikani mahala walipo.

Lakini kundi hilo liligawanyika mwaka 2016 na kupelekea kujitokeza kwa ISWAP ambalo hivi sasa linatawala katika mzozo unaoonekana wa kindugu kutokana na historia ya kundi.

Wafuasi wa Boko Haram walijaribu kufika kwenye maeneo yenye visiwa katika eneo la Ziwa Chad ambalo visiwa vyake vimekuwa kiini kwa wanajihadi.

XS
SM
MD
LG