Ongezeko hilo litaashiria mwisho wa utoaji ruzuku ya mafuta ambayo NNPC inasema inagharimu dola milioni 867 kwa mwezi, ambapo Rais mpya Bola Tinubu alisema Jumatatu itaufuta utaratibu huo wa ruzuku.
Wakati nchi hiyo inakabiliwa na hali ngumu ya uchumi, Wanigeria wengi wanaona kuwa wana haki ya kupata petroli kwa bei nafuu. Mara ya mwisho serikali ilipojaribu kuondoa ruzuku hiyo mwaka 2012, ilisababisha maandamano nchi nzima. Tinubu, ambaye wakati huo alikuwa kiongozi wa upinzani, alipinga kuondolewa kwa ruzuku hiyo.
Waraka wa NNPC ulitolewa baada ya taharuki iliyojitokeza ya ununuzi uliosababisha bei kupanda wakati Wanigeria wakikimbia kwenda kujaza matanki kabla ya kusitishwa kwa ruzuku ambayo ilikuwa ikisaidia kushusha bei ya mafuta.
Msemaji wa NNPC alikataa kutoa maoni.
Siku ya Jumanne, mtendaji mkuu wa kampuni ya NNPC alisema shirika hilo lilikuwa linadaiwa dola bilioni 6.1 ikiwa ni malipo ya ruzuku ya mafuta na serikali ya shirikisho na kwamba Nigeria haina uwezo tena wa kulipia ruzuku.
Vituo vinavyo uza mafuta yanayomilikiwa na NNPC katika baadhi ya maeneo ya Lagos, yalikuwa tayari yanauza petroli kwa naira 448 kutoka 185 kwa lita, wakati mjini Abuja ilikuwa inauzwa kwa naira 537.
Kupanda kwa bei ya petroli kutaongeza gharama za usafiri kwa wafanyakazi na biashara ndogo ndogo ambazo zinategemea majenereta, katika nchi hiyo yenye usambazaji mdogo wa umeme wa gridi.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters
Forum