Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:23

Bola Tinubu ameapishwa kama Rais ajaye wa Nigeria


Bola Tinubu, Rais mpya wa Nigeria
Bola Tinubu, Rais mpya wa Nigeria

Tinubu mwenye umri wa miaka 71 anatokea eneo la kusini anachukua madaraka kutoka kaskazini mwa nchi hiyo kwa mtangulizi wake mwenye umri wa miaka 80 wakati taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika likikabiliwa na matatizo ya kiuchumi na mzozo wa kiusalama

Mwanasiasa wa muda mrefu Bola Tinubu aliapishwa kuwa rais wa Nigeria leo Jumatatu akichukua nafasi ya Muhammadu Buhari, jenerali wa zamani ambaye ameondoka kwenye kiti hicho baada ya mihula miwili madarakani.

Tinubu mwenye umri wa miaka 71 anatokea eneo la kusini anachukua madaraka kutoka kaskazini mwa nchi hiyo kwa mtangulizi wake mwenye umri wa miaka 80 wakati taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika likikabiliwa na matatizo ya kiuchumi na mzozo wa kiusalama.

"Kama rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Nigeria nitatekeleza majukumu yangu na kuongoza kwa uaminifu kwa kadiri ya uwezo wangu, na kwa mujibu wa katiba", Tinubu alisema katika matangazo ya moja kwa moja kutoka eneo la Eagle Square katika mji mkuu Abuja.

Viongozi wa kigeni na wawakilishi waliokuwepo katika sherehe hizo ni pamoja na marais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Paul Kagame wa Rwanda na Nana Akufo-Addo wa Ghana, pamoja na wajumbe kutoka Marekani, Uingereza na China.

Forum

XS
SM
MD
LG