Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 17:14

Rais wa Nigeria azindua kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta


Kiwanda cha kusafisha mafuta katika jimbo la Kaduna, kaskazini magharibi mwa Nigeria.
Kiwanda cha kusafisha mafuta katika jimbo la Kaduna, kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari leo Jumatatu amezindua kiwanda cha mafuta kinachodaiwa kuwa kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta barani Afrika, baada ya uzinduzi huo kucheleweshwa kwa miaka kadhaa na wiki moja kabla ya rais kuondoka madarakani.

Kiwanda hicho cha kusafisha mafuta ambacho kilijengwa na tajiri mkubwa barani Afrika Aliko Dangote katika mji wa biashara wa Lagos, kina uwezo wa kusafisha mapipa 650,000 kwa siku, na kitaanzisha shughuli zake mwezi Juni.

Kwa miongo kadhaa, taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika na mzalishaji mkubwa wa mafuta ghafi limekuwa likitegemea mafuta yanayoagizwa kutoka nje ili kukidhi mahitaji ya ndani ya bidhaa hiyo kwa sababu ya viwanda vibovu vya serikali vya kusafisha mafuta.

Nigeria inabadilisha mafuta ghafi yenye thamani ya mabilioni ya dola kwa ajili ya petroli kisha kutoa ruzuku kwa ajili ya soko lake la ndani.

Hali hiyo ilisababisha upungufu mkubwa wa fedha za kigeni na kupungua kwa mapato kufuatia janga la Covid na vita kati ya Russia na Ukraine.

XS
SM
MD
LG