Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:13

Dangote ajenga kiwanda kikubwa cha mafuta Afrika


Kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote huko Lagos, likichozinduliwa na rais wa Nigeria Muhammadu Buhari tarehe 22, Mei 2023. Picha na PIUS UTOMI EKPEI /AFP.
Kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote huko Lagos, likichozinduliwa na rais wa Nigeria Muhammadu Buhari tarehe 22, Mei 2023. Picha na PIUS UTOMI EKPEI /AFP.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari Jumatatu amezindua kiwanda cha mafuta kinachoelezewa ni kikubwa sana barani Afrika, baada ya uchelewesho wa miaka mingi na wiki moja kabla ya kuachia madaraka.

Kiwanda hicho ambacho kimejengwa na tajiri mkubwa sana barani Afrika Aliko Dangote, kiko katika kitovu cha kibiashara kwenye jiji la Lagos, kiwanda hicho cha kusafishia mafuta – kina uwezo wa kusafisha mapipa 650,000 kwa siku -- kinatarajiwa kuanza kazi mwezi Juni.

Kwa miongo kadhaa, taifa hilo lenye watu wengi sana barani Afrika na pia ni moja ya wazalishaji wakubwa sana wa mafuta ghafi barani humo limekuwa likitegemea uagizaji bidhaa kutoka nje ili kukidhi mahitaji ya ndani kwa sababu mitambo ya kusafisha mafuta inayoendeshwa na serikali kushindwa kufanya kazi vizuri.

Nigeria ina uwezo wa kusafisha mafuta ghafi yenye thamani ya mabilioni ya dola kwa ajili ya petroli na baadaye kutoa ruzuku kwa soko lake la ndani.

Uagizaji wa mafuta, umesababisha upungufu mkubwa wa fedha za kigeni wakati mapato ya mafuta yalipopungua kufuatia janga la virusi vya COVID na vita vya Russia na Ukraine.

Kiwanda hicho kipya, kimejengwa kwenye eneo la hekta 2,635 za ardhi huko Lekki Free Zone na kugharimu wastani wa dola bilioni 19, kulingana na vyombo vya habari vya Nigeria, Ujenzi wa kiwanda hicho unaweza kuwa ni hatua muhimu.

Kiwanda cha kusafisha mafuta, ambacho kilipangwa kufunguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2021, "itapunguza mtiririko wa fedha za kigeni" na "kufungua nafasi nyingi za ajira," meneja mkuu wa kampuni ya Dangote ambaye hakutaka jina lake litajwe aliliambia shirika la habari la AFP.

Alisema mradi huo "utakidhi mahitaji yote ya Wanigeria," na kutoa kukidhi mahitaji ya sehemu mbalimbali duniani.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP .

XS
SM
MD
LG