Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:52

Washambuliaji wenye silaha waua watu 30 kaskazini mwa Nigeria


Ramani ya Nigeria
Ramani ya Nigeria

Watu wenye silaha waliua watu 30 katika mashambulizi ya mwishoni mwa Jumaa kwenye vijiji sita kaskazini mwa Nigeria, eneo ambalo hukumbwa mara kwa mara na ghasia za uhalifu na mapigano kati ya jamii, polisi wa jimbo hilo wamesema.

Watu hao waliuawa na watu waliokuwa wanaendesha pikipiki, msemaji wa polisi wa jimbo la Sokoto, Ahmad Rufai alisema Jumatatu katika taarifa.

Hata hivyo, wakazi kutoka vijiji viwili kati ya vilivyoshambuliwa wamesema watu 36 ndio waliuawa katika mashambulizi ambayo wanasema ni ya kulipiza kisasi kwa kupinga kulipa pesa za kuwalinda dhidi ya majambazi.

Mkazi wa kijiji cha Raka, Kasimu Musa, ameiambia AFP “ Tulizika watu 36 jana Jumapili ambao waliuawa na majambazi.”

Ghasia za kijamii ni moja ya changamoto za kiusalama zinazomkabili Rais Bola Tinubu aliyeapishwa wiki iliyopita baada ya kushinda uchaguzi wa mwezi Februari uliogubikwa na tuhuma za wizi wa kura zilizotolewa na vyama vya upinzani.

Forum

XS
SM
MD
LG